Tuesday, 24 April 2018

Ushirikiano wa kihistoria baina ya Tanzania na Israel kuimarishwa

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na wanahabari baada ya kuzindua rasmi Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Israel (TIBIF) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Sheria wa Israel, Ayelet Shaked na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Felix Mosha.

Waziri wa Sheria wa Israel, Ayelet Shaked akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Israel (TIBIF), jijini Dar es Salaam. 


Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Israel (TIBIF) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (hayupo pichani) alipokuwa akizindua kongamano hilo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Waziri wa Sheria wa Israel, Ayelet Shaked walipokutana jijini Dar es Salaam. Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. 


Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akiteta jambo na Waziri wa Sheria wa Israel, Ayelet Shaked walipokutana jijini Dar es Salaam. Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Kushoto ni Balozi wa Israel anayehudumia Afrika Mashariki, Noah Gal Gendler.


Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Sheria wa Israel, Ayelet Shaked (kushoto) walipokutana kwa ajili ya mazungumzo jijini Dar es Salaam. Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Kutoka kulia ni Mtetezi Mkuu wa Serikali ya Israel, Dk. Yoav Sapir, Balozi wa Tanzania nchni Israel, Job Masima.


Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Adelardus Kilangi akiteta jambo na Waziri wa Sheria wa Israel, Ayelet Shaked walipokutana Dar es Salaam. Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Sheria wa Israel, Ayelet Shaked (waliokaribu na bendera) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Israel (TIBIF) mara baada ya kuzinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija – Maelezo)

No comments:

Post a Comment