Friday, 20 April 2018

Virutubisho vinavyotokana na mimea msaada kwa wenye uvimbe katika kizazi


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akielezea tatizo la uvimbe katika kizazi linalowakabili kinamama huku akiwa ameshika moja ya virutubisho kinachosaidia kupambana na matatizo mbalimbali ya kiafya.MOJA ya matarajio ambayo mama mjamzito anayatazamia ni kuzaa salama mtoto wake tena asiye na kasoro.

Kwa kawaida mama hubeba mimba kwa muda wa miezi tisa, lakini anaweza kujifungua zaidi ya muda huo ama kabla kutokana na sababu mbalimbali.

Zipo sababu nyingi ambazo zinazoweza kusababisha mama mjamzito kuzaa mtoto mfu ama kupata matatizo mengine yanayoweza kufifisha matarajio hayo.

Tatizo la kuharibika mimba linatokana na sababu nyingi ikiwemo mfadhaiko wa kiajali au sababu za kimaumbile.

Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai, anasema uvimbe katika kizazi ni miongoni mwa sababu kubwa ambazo huchangia mimba kuharibika.

"Uvimbe katika tumbo la uzazi ni moja ya sababu ambazo humweka mwanamke katika hatari ya mimba kuharibika kwani unaweza kujaa kwenye sehemu anayokaa mtoto," anasema.

Anabainisha kuwa ugonjwa wa fibroids yaani uvimbe katika kizazi, huwa kwenye ukuta wa kizazi ambapo mwanamke anaweza kusaidiwa kwa kupatiwa virubisho tiba vinavyoandaliwa kwa kutumia mimea na mwathiriwa akaondokana na tatizo hilo.

Mtaalam huyo anafafanua kuwa uvimbe unaweza kuwa mdogo kama ncha ya kidole au mkubwa kama kiazi. Unaweza kugunduliwa kwa kutumia kipimo kinachojulikana kitaalamu kama ultrasound.

Anatanabaisha kuwa ugonjwa huo unaweza kumpata mwanamke yeyote mwenye umri wa kuzaa lakini wanawake ambao hubalehe mapema miaka 11 au chini ya umri huo, wapo katika hatari kubwa zaidi ya kuupata.

Mandai anasema dawa za kuongeza makalio, matiti na za kuchubua ngozi zinamweka mwanamke katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya uvimbe katika kizazi.

Aidha, anatanabaisha kuwa zipo aina nyingi za uvimbe lakini saba ndizo hujulikana zaidi huku dalili zake ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi na kichefuchefu cha daima.

Pia nyonga huuma hasa pale mwanamke anapofanya kazi nzito kama kuinua mzigo huku wakati mwingine hujisikia tumbo kujaa.

Mtaalamu huyo anaendelea kufafanua kuwa ugonjwa huo unatibika hospitali ambapo moja ya matibabu yake ni kwa kufanyiwa upasuaji kwa kuondoa eneo lenye uvimbe.

Anasema ingawa kuna aina za upasuaji zinazotumiwa kuondoa fibroids lakini tiba mbadala ni nzuri zaidi kwani mtu anapofanyiwa upasuaji kuna uwezekano wa uvimbe huo kujirudia.

"Ingawa kuna aina za upasuaji zinazotumiwa ili kuondoa fibroids lakini tiba mbadala ni nzuri zaidi kwani unapofanyiwa upasuaji kuna uwezekano wa uvimbe kujirudia. Na tiba hiyo haina madhara kwa mgonjwa," anasema.

Anafafanua kuwa kuna upasuaji ambao mwanamke hutolewa kizazi chote na kwamba baada ya hapo uwezekano wa kushika mimba ni mdogo.

"Hata hivyo, kuna upasuaji ambao mgonjwa anatolewa kizazi chote hatua hiyo inamfanya asiweze kutunga mimba tena. Hii hufanywa kwa mwanamke ambaye eneo lote la kizazi limezungukwa na uvimbe,"anasema.

Mtaalamu huyo anashauri kinamama kupata vipimo hospitali mara tu wanabaini wana maumivu ya tumbo yasiyo ya kawaida hasa katika kipindi cha hedhi.

Aidha, anaweka wazi kuwa tatizo hilo kwa wanawake kwa sasa ni kubwa kutokana na matumizi makubwa ya vipodozi na dawa za kuongeza matiti na makalio.

Anasema mwanamke mwenye tatizo hilo ambaye anachelewa kupata tiba anakuwa katika hatari ya kupata saratani ya kizazi ambayo inaweza kusababisha kifo ama hata kutowajibika ipasavyo katika kazi za ujenzi wa taifa.

Pamoja na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kuwa miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo kwa wanawake nchini, inaaminika kuwa ni asilimia 66 tu ya wanawake wa miaka kati ya 15 na 49 wana taarifa sahihi kuhusu ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road mwaka 2011, Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki kwa kuwa na wagonjwa wengi wa aina hiyo ya saratani.

Kutokana na matokeo hayo Tanzania ina wastani wa wagonjwa 50 kwa kila wanawake 100,000 wa saratani ya shingo ya uzazi.

Utafiti huo pia unaonesha kuwa kwa mwaka 2011 wastani wa vifo kutokana na ugonjwa huo ilikuwa 37.5 kwa kila wanawake 100,000 na katika wagonjwa wote wa saratani waliotibiwa Ocean Road, asilimia 36 waliugua saratani ya shingo ya kizazi.

Tume ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika utafiti wake uliofanyika kati ya mwaka 2011 na 2012, inabainisha kuwa ukosefu wa elimu na kipato duni ni miongoni mwa sababu zinazochangia wanawake wengi kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu ugonjwa huo.

Utafiti unaonesha kuwa asilimia 52 ya wanawake wasiokuwa na elimu ya sekondari na chuo kikuu, ndio walipata taarifa kuhusu ugonjwa huo huku asilimia 75 ya wanawake wasomi walikuwa na taarifa sahihi.

Tafiti zinasema ukaaji wa mijini na vijijini pia unachangia hali hiyo, kwani wanawake wengi wa mjini wana fursa ya kupata taarifa kutokana na urahisi wa kufikiwa na vyombo vya habari tofauti na wenzao wa vijijini.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho tiba vinavyozalishwa na kampuni yetu.

No comments:

Post a Comment