Wednesday, 25 April 2018

Vyakula hivi vinasaidia wenye virusi vya Ukimwi kuimarisha miili yao
UGONJWA wa Ukimwi ni moja ya magonjwa hatari hapa nchini, katika nchi nyingine za Afrika na duniani kwa ujumla.

Ni ugonjwa hatari kwa sababu tangu ungundulike zaidi ya miongo mitatu iliyopita, hauna dawa ambapo wataalam wanaendelea kutafuta dawa ya maradhi hayo hadi sasa hawajafanikiwa.

Zipo dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo ambazo kama nilivyosema hapo awali ni za kupunguza makali tu na si kutibu ambazo mgonjwa analojukumu la kuzitumia katika maisha yake yake yote.

Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai anasema virusi vya ugonjwa huo hurutubishwa au kupunguzwa nguvu kutokana na vyakula anavyokula mgonjwa husika.

Mandai anasema kwa kuwa ugonjwa huo unaharibu kinga ya mwili na hivyo kuudhoofisha mwili wa mgonjwa husika, mwathirika anapaswa kutumia vyakula vinavyoongeza kwa wingi kinga za mwilini na kufukuza magonjwa.

Anafafanua kuwa asali ni nzuri katika kupambana na ugonjwa huo na mengine, itumike kama sukari katika chai pia itumike kama chakula au siagi katika mkate au mgonjwa anaweza kuitumia kwa kuilamba.

Anabainisha kuwa asali ni nzuri kwa watu wote hata kwa wasioathirika pia ni kinga nzuri kwa magonjwa mbalimbali.

Anasema mtu anayejiwekea utaratibu wa kulamba asali anajiweka katika uwezekano wa kuepuka magonjwa lakini pia ni tiba nzuri kwa vidonda katika mwili wa binadamu.

Mtaalam Mandai anasema chakula kingine kinachoweza kumweka katika hali nzuri mgonjwa wa Ukimwi ni soya.

Anatanabaisha kuwa mgonjwa anatakiwa kutumia mazao ya soya kwa namna mbalimbali kama sehemu ya kuujenga mwili wake kuwa wenye afya njema na nguvu.

"Tengeneza juisi ya aloevera, au nunua aloevera iliyochunjwa kutoka kwa wataalam wa miche na kutumia dozi hiyo kwa muda wa siku tano kila mwezi mara moja endelea hivyo, utasahau na kujihoji ulichodhoofika kabla hujaanza kutumia dawa hiyo.

"Kazi mojawapo ya aloevera ni kuongeza askari wa kulinda mwili, nyingine ni kuongeza siku za kuishi kwa wagonjwa wa Ukimwi," anasema mtaalam  huyo.

Si hivyo tu, Mandai anawataka waathirika wa ugonjwa huo kutumia uyoga kila mara kama mboga za kawaida huku akiwasisitiza walaji kuepuka uyoga wenye sumu.

Katika hilo anafafanu kuwa kuna uyoga aina mbili za uyoga,  wakupandwa na ule wa pori ambao huota wenyewe kipindi cha mvua za masika nao una faida kubwa kwa mwathirika katika kulinda mwili wake.

Mtaalamu huyo anasema mwathirika ni vema akaepuka kula baadhi ya vyakula kama nyama.

"Nyama inasifika kwa kuwa na protini nyingi, ina uwezo mkubwa wa kuwarutubisha virus hawa wa Ukimwi. Kitaalam virusi hawa pia wamefunikwa na lea ya protini juu ya  mgongo wao," anasema.

Mandai anafafanua kuwa virusi hao kiasili makao yao ni katika wanyama na kwamba binadamu amehamishiwa tu, hivyo kuepuka nyama ni kuwakosesha lishe bora.

Pia anaonya waathirika waepuke kula sukari nyeupe inayotokana na miwa kwa kuwa inasifika kwa kuleta magonjwa katika mwili wa binadamu na kwamba matumizi yake yanaweza kuongeza nguvu kwa virusi hao kujiimarisha zaidi.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vinavyozalishwa na kampuni yetu.

No comments:

Post a Comment