Tuesday, 10 April 2018

Wafungwa wafurika baadhi ya magereza nchiniWafungwa waliposhiriki maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani mwaka 2013 kwenye gereza Kuu la Ukonga (PICHA YA MAKTABA)

Peter Simon

TANZANIA inakadiriwa kuwa na wafungwa 40,000 wakati uwezo wa magereza yake ni kuwa nao 30,000 hivyo kuna ongezeko la zaidi ya wafungwa 10,000 katika msongamano huo.

Kauli hiyo imetolewa jana bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusufu Masauni wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge, Ruth Mollel ambaye ametaka kujua Serikali inafanya nini kumaliza msongamano wa wafungwa katika magereza mbalimbali nchini.

Masauni amesema kuna ongezeko la zaidi ya wafungwa 10,000 ambapo kwa sasa Serikali inafanya kila namna kumaliza msongamano huo.

Katika swali la msingi mbunge wa Bububu, Mwantakaje Haji Juma  (CCM) amehoji ni lini kituo cha polisi katika jimbo lake kitafanyiwa ukarabati.

Naibu Waziri amesema kituo hicho kitafanyiwa kazi wakati wowote fedha zikipatikana ili kiwawezeshe askari kutoa huduma bora.

No comments:

Post a Comment