NYANYA ni kiungo maarufu hapa nchini na maeneo mengi
Afrika Mashariki na duniani kote. Asili ya mnyanya ni Amerika Kusini huku historia
ikionesha kuwa mmea huo ulianzia huko Peru.
Kiungo hicho licha ya kuongeza radha nzuri katika vyakula pia
kinasaidi pia jamii kuondokana na matatizo mbalimbali ya kiafya.
Miongoni mwa maradhi ambayo nyanya inasaidia kupambana
nayo ni pamoja na kupooza, inaondoa mafuta katika damu na kukabili tatizo la kumbukumbu.
Mtaalamu wa mimea wa kifaransa, Joseph Pitton de Tournefort,
alitoa jina la kisayansi ’Lycopersion esculum’ kwa nyanya, na wakati huo nyanya
ilifikiriwa kuwa ina sumu ndiyo maana ilipewa jina la mito lenye maana ya tunda
la mbwa mwitu.
Watu wa Acret na wengine walianza kutumia nyanya kwenye
mapishi yao, wakati huo ikilimwa huko Peru, mnamo mwaka 500KK.
Unaweza
kuitumia nyanya kwa kula baada ya kuiunga katika mboga, kunywa juisi yake, pia
inatumika tengenezewa kiungo maarufu kinachojulikana kama sosi ya nyanya
(tomato sosi) na uji mzito wa nyanya (tomato paste) ambavyo vina faida kubwa
katika mwili wa binadamu.
Uwezo
mkubwa wa nyanya katika tiba unatokana na kuwa na kiwango cha nyuzinyuzi ambazo
zinasaidia katika baadhi ya maradhi yanayozikabili jamii nyingi sasa.
Hata
hivyo, iwapo utakabiliwa na tatizo la kiafya, ni vema ukaja makao yetu makuu
kupata maelezo ya kina ya namna ya kutumia nyanya na matunda mengine.
Mchanganuo
huu umeletwa kwako na mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.
Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya
karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na
Mtaalam Mandai kwa simu
+255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri
au virutubisho vyetu.
No comments:
Post a Comment