Sunday, 22 April 2018

Wakili aliyemtusi Rais Magufuli akiona cha moto


Rais Dk. John Magufuli

Peter Simon, Dar es Salaam

WAKILI wa kujitegemea, Leonard Kyaruzi amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh. milioni 5 baada ya kukutwa na hatia ya
kumkashifu Rais Dk. John Magufuli kwa kumwita zuzu.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu mkazi Kisutu, Godfrey Mwambapa, baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wanne wa Jamhuri na utetezi wa mshtakiwa.

Katika hukumu hiyo, hakimu aliegemea katika maelezo yake ya onyo ambayo yamepita bila kupingwa kama kielelezo cha upande wa Jamhuri mahakamani hapo.

"Mahakama hii bila kuacha shaka imepitia ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa Jamhuri, imekuona una hatia, utalipa faini ya sh. milioni 5 ukishindwa utakwenda jela miaka mitatu," amesema hakimu Mwambapa.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Juni 2, 2016 katika jengo la Tanzanite lililopo Barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam,  mshtakiwa alichapisha taarifa kwenye mtandao wa Whatsapp kwa lengo la kumkashifu Rais Magufuli.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alichapisha taarifa za matusi ambapo mahakama ilithibitisha kosa hilo.

No comments:

Post a Comment