Friday, 20 April 2018

Wayajua maajabu ya mbuyu kwa afya yako?


Mbuyu

NCHINI na duniani kote kuna aina nyingi ya miti inayosaidia kwa waliokumbwa na matatizo mbalimbali ya kiafya. Ipo miti inayosaidia maradhi ya tumbo na tumbo la uzazi, mingine hutibu kichwa, miguu, mikono hata uvimbe unaojitokeza katika mwili.

Ninapozungumzia kuhusu mimea tiba, matabibu waliobobea katika fani hiyo nawafikisha mahali pao kwa sababu wao wanaiona mimea hiyo katika fikra zao.

Mbuyu ni miongoni mwa mimea tiba ambao unastawi katika maeneo yenye ukame. Mti huu hutumika katika kusaidia matatizo mbalimbali ya kiafya, lakini vilevile kama chakula, hutoa maji lakini pia hutumika kupumzikia viumbe mbalimbali wakiwemo binadamu na wanyama.

Wanyama wa mwituni hupumzika kutokana na kivuli cha mti huo kwa sababu huota wenyewe tena sehemu yoyote hata kama ni porini.

Mibuyu imeenea katika maeneo mengi nchini licha ya mikoa ya ukanda wa kati kama Tabora, Dodoma, Singida na Iringa, lakini pia mikoa ya mwambao mwa Bahari ya Hindi kama Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga.

Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai anasema katika kipindi cha miaka mingi mbuyu umekuwa ukitumika kama chakula (mboga za majani) na unga wa tunda la mti huo hutumika kama kinywaji na dawa.

Anasema majani yake yamesheheni virutubisho vingi ikiwemo Vitamini C, sukari na madini ya chokaa. Anatanabaisha kuwa majani ya mti huo hupikwa na kuliwa kama mboga nyingine za majani.

Anasema mbegu za mmea huo huliwa baada ya kukaangwa pia zinaweza kutwangwa na kupata unga unaoweza kutumika kutengeneza kinywaji kama ilivyo kwa kahawa.

"Unga wa majani ya mbuyu umesheheni wanga, nyuzi, chokaa, fosforasi, vitamini C na A. "Pia una asilimia 4.36 ya hamirojo, asilimia 22.62 ya wanga, miligramu 88.61 za chokaa (Ca), miligramu 102.27 ya fosforasi (P) na 43.80 ya vitamini A," anasema mtaalamu huyo.

Anaongeza kuwa mbuyu ukikaushwa huwa na kemikali kama proline, histidine, leucine, lysine, arginine, isoleucine, methionine, cystine, phenilalane, Glutamic acid, valine, tyrosine, tryptophan na threonine.

Anasema katika gramu 100 za unga wa mbuyu una glucose, frustose, scrose, maltose, soluble, polysaccharides na mafuta. Kwenye mbuyu pia kuna madini kama potassium, sodium, calcium na iron.

"Kwa hiyo ni wazi kuwa mbuyu ni mmoja kati ya miti yenye faida kubwa kwa jamii na unaweza hata kutumika kama moja ya zao la biashara ndani na nje ya nchi," anabainisha.

Anafafanua kuwa gome la mti huo unaodaiwa kuishi miaka kati 150 hadi 400 lina unene wa milimita 50 hadi 100 ambapo majani yake hufanana na kiganja chenye vidole vitano hadi saba.

Pia mbuyu hutoa maua meupe makubwa matamu huku yakiwa tiba ya magonjwa mengi. Anasema matunda ya mmea huo maarufu nchini na katika maeneo mengine ambayo yana asili ya jangwa, ni mviringo kama yai, lakini pia ukubwa wake ni zaidi ya milimita 120.

Tunda la mbuyu lina ngozi ngumu na ndani kuna unga mweupe wenye mbegu ngumu, nyeusi, zenye umbo la figo.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vinavyozalishwa na kampuni yetu.

No comments:

Post a Comment