Monday, 9 April 2018

Waziri ataka waliovamia Ngitili kuondoka mara moja


Dk.  Hamisi  Kigwangallah 

Mwandishi Wetu, Shinyanga

WAZIRI wa  Maliasili  na  Utalii,  Dk.  Hamisi  Kigwangalla  ametoa  siku 30 kwa wote waliovamia  hifadhi  ya  mistu  maarufu  kama  ‘Ngitili’  kuondoa haraka.

Hatua hiyo inalenga kukabiliana na uharibifu wa mazingira uliosababishwa na watu kuvamia  mistu  hiyo  chini  ya  Mradi  wa Hifadhi  Aridhi  Shinyanga (Hashi).

Waziri huyo ametoa kauli hiyo hivi karibuni wilayani Kishapu wakati wa kilele cha wiki ya  upandaji  miti  nchini  ambapo  kitaifa  ilifanyika  mkoani  Shinyanga.

Amesema ngitili zilianizshwa ili kuresha  uoto  wa  asili  mkoani  humo  lakini baadhi  watu  wachache  wasioitakia  mema  Shinyanga  wameingia  maeneo hayo na kujimilikisha  huku  wakiendesha  shughuli  ambazo  ni kinyume cha uhifadhi wake.

Dk. Kigwangalla amesema baada ya siku hizo kumalizika kama wahusika hawatakuwa wameondoka  wenyewe  kwa  hiari  itabidi  nguvu  itumike  kuwaondoa kunusuru uharibifu usiendelee.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema wataendelea kutoa elimu kwa  wananchi  kuhusu madhara  ya  uvamizi  wa  hifadhi za mistu.

Amesema sanjari na hilo ametoa  mwito  wa  kuimarisha  nguvu  katika  matumizi  majiko yanayotumia nishati kidogo na yale ya  gesi  ili  kunusuru mistu nchini.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack naye amewataka  watendaji  wote  kuanza kuwaondoa wavamizi wa vyanzo vya maji na misitu.

Aidha ameomba juhudi za usambazaji wa gesi kwa ajili ya kupikia vijijini uongezwe ili kuwasaidia  wananchi  kuachana  na  matumizi  ya  mkaa  na kuni ambazo zinachangia kumaliza mistu.

Naye Meneja wa Wakala wa Mistu Tanzania(TFS), Kanda ya MagharibiValentine Msusa amesema  wanayo  orodha  ya  Ngitili  zote  zilizokuwa  zimehifadhiwa chini ya mradi Hashi na wanatarajia  kukikabidhi  kwa uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya hatua zaidi.

Maadhimisho ya mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu; Tanzania ya kijani inawezekana , panda miti kwa maendeleo ya viwanda.

No comments:

Post a Comment