Tuesday, 3 April 2018

Waziri mkuu: Endeleeni kusajili wanunuzi wa pambaWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Mwandishi Wetu, Mwanza

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa mkoa wa Mwanza kuendelea kusaji wanunuzi wa zao la pamba na wawape fursa ya kuchagua maeneo wanayotaka kununua malighafi hiyo.

Ametoa kauli hiyo  alipozungumza na viongozi mkoa wa Mwanza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege  wa Mwanza akiwa njiani kuelekea mkoani Geita.

Waziri Mkuu jana alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuwasha mwenge wa Uhuru mkoani Geita. Kauli mbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’

Waziri Mkuu amesema wakati viongozi hao wakiendelea na usajili wa wanunuzi wa pamba ni vema wakawapa nafasi ya kuchagua maeneo watakayohitaji kukunua kwa sababu yanaweza kurahisisha usafirishaji.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi hao kuendelea kusimamia na kufuatilia maendeleo ya zao hilo kwa umakini zaidi ili kuweza kubaini changamoto zitakazojitokea na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati.

Amesema kutokana na mwenendo wa hali ya hewa mwaka huu wakulima wa zao la pamba wanatarajiwa kuvuna pamba nyingi, hivyo ni vema ukatengenezwa utaratibu utakaomrahisishia mkulima kutoa mazao shambani na kufikisha mnadani.

Waziri Mkuu amesema utaratibu huo wa kutoa mazao shambani na kupelekwa mnadani kwa wakati ni muhimu kwa sababu utasaidia katika kulinda pambaisipoteze ubora wake.

Zao la pamba ni miongoni mwa mazao matano ya biashara ambayo Serikali imeamua kuyapa kipaumbe kwa kuyafuatilia kuazia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba, pembejeo pamoja na uuzaji. Mengine ni korosho, chai, kahawa na tumbaku.

No comments:

Post a Comment