Tuesday, 10 April 2018

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga akizungumza na mgeni wake Balozi wa Hispania nchini, Felix Artieda

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga akifafanua jambo kwenye mazungumzo na Balozi wa Hipania nchini, Felix Costales Artieda alipomtembelea Wizarani jana Aprili  09, 2018, Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalijikita katika kuzidi kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Hispania.
Balozi Felix Costales Artieda (kushoto) akieleza jambo kwa Waziri Dk. Augustine Mahiga kwenye mazungumzo hayo. Mazungumzo yakiendelea, wanaoshuhudia mazungumzo hayo ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Salvatory Mbilinyi(kulia katikati),Katibu wa Waziri Magabiro Murobi (Kulia mwisho)na kushoto ni Naibu Balozi Teresa Martin. Balozi Felix Costales Artieda (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  mwenyeji wake Dk. Augustine Mahiga jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment