Thursday, 26 April 2018

Ziara ya naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye jimboni kwake Mhambwe Kigoma,


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akipokea kompyuta 25 zenye thamani ya shilingi milioni 45 kutoka kwa Mkuu wa Operesheni wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), zilizotolewa na mfuko huo kwa ajili ya shule za sekondari za jimboni kwake Muhambwe, Kibondo mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mkuu wa shule ya sekondari ya Mkugwa Salome (kushoto) kuhusu mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya masomo ya sayansi kwenye moja ya maabara za shule hiyo jimboni kwake Muhambwe, Kibondo mkoani Kigoma.


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akikagua mabweni kwenye shule ya sekondari ya wasichana ya Mkugwa wakati wa ziara yake shuleni hapo.


Nembo ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), iliyowekwa kwenye kompyuta 25 zenye thamani ya sh. milioni 45 zilizotolewa kwa naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye kwa ajili ya shule za sekondari zilizopo jimboni kwake Muhambwe, Kibondo mkoani Kigoma.


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Boni Consilii alipowasili kuzungumza nao wakati wa ziara yake jimboni kwake Muhambwe, Kibondo mkoani Kigoma.

No comments:

Post a Comment