Sunday, 29 April 2018

Zimbabwe yahalalisha ukulima wa bangi


Bangi inavyostawishwa
ZIMBABWE imehalalisha uzalishaji wa bagi kwa matumizi ya kiafya na kisayansi.
Inakuwa nchi ya pili kufanya hivyo barani Afrika baada ya Lesotho iliyotoa leseni yake ya kwanza kwa kilimo cha mmea huo mwaka uliopita.
Serikali ya nchi hiyo imesema watu nchini Zimbabwe sasa wanaweza kutuma maombi ya kustawisha zao la bangi.
Hadi sasa, banki ilikuwa ni zao haramu kupanda, kumiliki au kutumia nchini humo ambapo yeyote ambaye alikutwa na hatia alikuwa akihukumiwa kifungo cha hadi miaka 12 gerezani.
Waziri wa afya wa nchi hiyo, David Parirenyatwa alichapisha sheria zinazowaruhusu watu na kampuni kupewa leseni ya kustawisha bangi ambayo hufahamika nchini humo kama mbanje.
Leseni hiyo inatakiwa iombwe upya kila baada ya miaka mitano na itawaruhusu wakulima kumiliki, kusafirisha na kuuza zao hilo.
Watuma maombi watatakiwa kueleza ni wapi watafanyia kilimo chao, kiwango ambacho wataweza kuzalisha na kuuza na wakati gani wa kuzalisha bangi hiyo.

No comments:

Post a Comment