Thursday, 5 April 2018

Zitto kumsindikiza Nondo uhamiaji


MBUNGE wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amesema atamsindikiza kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Abdul Nondo makao makuu ya uhamiaji.
Ametoa kauli hiyo baada ya taarifa iliotoka kutoka mtandao huo ambao ulieleza kuwa Nondo alipata barua ya kuitwa na uhamiaji ili akahojiwe kuhusu taarifa za uraia wake pamoja na za ndugu zake.

Zitto Kabwe
Barua hiyo imesema ofisa uhamiaji mkoa alitamka kuwa sheria inawaruhusu kumhoji mtu yeyote wanayemtilia shaka uraia wake, na hivyo wana shaka na uraia wa Nondo,hivyo awathibitishie iwapo yeye ni raia wa Tanzania au la.
Nondo anashatakiwa kwa kosa la kudanganya kuwa alitekwa na kudaiwa kutoa taarifa za uongo mtandaoni.
Taarifa za kupotea kwa Nondo katika mazingira ya utata ziliibuka Machi6, mwaka huu  baada ya Nondo kutuma ujumbe kwa mmoja wa marafiki zake usiku wa manane akisema kuwa usalama wake uko hatarini.
Hali hiyo ilipeleka taharuki miongoni mwa wanafunzi wenzake na jamii kwa ujumla huku wengi wakidhani kuwa Nondo alikuwa ametekwa.
Sasa Nondo anatakiwa kurudi uhamiaji Aprili 20 na kupeleka cheti chake cha kuzaliwa, cheti cha kuzaliwa cha baba yake, mama yake, cha bibi na babu mzaa baba na mzaa mama.

Abdul Nondo

No comments:

Post a Comment