Tuesday, 1 May 2018

ACT Wazalendo yawataka wanachama wake kutembea kifua mbele


Claudia Kayombo

CHAMA cha ACT Wazalendo kimewataka wanachama wake kutembea kifua mbele huku wakijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chama hicho.

Katibu mkuu wa chama hicho, Doroth Semu ametoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza katika mkutano wa ndani wa chama hicho, uliolenga kukutana na kuwapokea wanachama wapya zaidi ya 100 waliopatikana katika kipindi cha kati ya Januari ya                                           Aprili mwaka huu katika mkoa wa                                             Dar es Salaam.

Doroth Semu

“ACT Wazalendo tunaamini kuwa kila mtu anawajibu wa kuchangia katika chama, vijana na wanawake tembeeni kifua mbele na mjitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi,”amesema.

Amesema chama hicho kinajali utu wa kila mtu, hivyo kila mwanachama ajione ni sehemu ya chama hicho hata kama ana siku mbili tangu ajiunge nacho.

No comments:

Post a Comment