Friday, 25 May 2018

Alishtaki kanisa kwa kumuwekea masharti makali ya kufunga ndoa


Michael Aboneka
MWANAUME mmoja amelishtaki kanisa moja nchini Uganda akipinga kanuni za utaratibu wa kufunga ndoa akieleza kuwa zinakwenda kinyume na katiba.
Michael Aboneka amepeleka kesi hiyo katika mahakama ya katiba mjini Kampala kulishtaki Kanisa la Watoto wakati waumini wengine wa kanisa hilo wakiunga mkono taratibu za kanisa lao.
Michael Aboneka amesema kuwa Watoto Church, linawanyima vijana wengi haki yao ya kikatiba ya kufunga ndoa na wapenzi wao baada ya kutimiza umri wa miaka 18 kama katiba ya Uganda inavyosema.
Ameeleza kuwa baada ya kuzisoma kanuni hizo za kufunga ndoa, ameona kuwa zinakwenda kinyume na katiba.

'Kwanza wanasema nilazima upate barua kutoka kwa wazazi wa bibi harusi ambayo wanaita Baraka. Kwangu inakwenda na kinyume cha katiba kifungu 31 ya ndoa ya pili ni kukabidhi barua ya Dakitari ya majibu ya kupima virusi vya ukimwi kwa kanisa'.
'Nimekwenda hospitalini kupimwa na mchumba wangu tumepata majibu tunafahamu majibu ya kila mmoja wetu. Kwa hiyo mimi na mchumba wangu kukabidhi vipimo vya ukimwi kwa kanisa inavunja haki ya uhuru wa siri zetu, nimekuta ni kinyume na katiba'. amesema Aboneka.
Aboneka ameongeza kuwa kununi nyingine ambazo anaziona kama kero ni kusubiri kwa mda wa miezi sita baada ya kuomba kufanya harusi na kulipa ada katika kanisa shilingi lakini nne na nusu za Uganda sawa na dola 130.
Lakini kwa waumini wa kanisa hilo wao waanasema hakuna tatizo.
Ndio naunga mkono sheria na taratibu za kufunga ndoa katika kanisa la watoto, kwa sababu kila jamii wana taraibu zao na sheria zinazowaongoza, amesema Vanesa Naluwoga.
'Hivyo nina unga mukono. Na mimi mwenyewe nilifunga ndoa tarehe 27 Octoba 2012 kwa kupitia taratibu hizo zote tulizoambiwa', ameongeza Naluwoga.
Michael Aboneka ameongeza kusema kuwa siyo kanisa la watoto pekee lenye utaratibu huo bali makanisa mengi nchini yanafanya hivyo na anasema ameiomba mahakama ya katiba kuanza mara moja kusimamisha kanuni hizo na anatarajia wiki hii mahakama inaweza kutoa jibu.
Aboneka amesema kuwa siyo kwamba ana chuki na kanisa la watoto, ila ni kusaidia vijana wengi ambao wameshindwa kufunga ndoa zao ili mahakama ya katiba itoe ufumbuzi wa suala hilo.

No comments:

Post a Comment