Friday, 25 May 2018

Alizeti ni tiba ya mishipa ya fahamu


Kilimo cha alizeti

ZAO la alizeti hustawishwa ili kupata mafuta ya kupikia yanayotokana na mbegu,  yanaaminika sana kwa kuwa hayana lehemu (cholesterol) . Wengine hutumia mbegu hizo kama kiungo baada ya kuzitwanga au kusaga.

Alizeti inastawishwa katika maeneo mengi hapa nchini, huku mikoa ya kati, kwa maana ya Dodoma, Singinda, Shinyanga, Tabora na hata ile ya Simiyu, Geita na Mwanza inastawisha kwa wingi zaidi.

Wakati zao hili likistawishwa kama kiungo, pia lina uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi mbalimbali kuanzia majani, maua hadi mizizi.

Majani au maua ya alizeti yakichemshwa na kunywewa kama chai ni tiba ya maradhi ya kuhara, mapafu, vikohozi na pumu.

Juisi inayotengenezwa kutokana na mbegu zake mbichi ni tiba ya mishipa ya fahamu, mapafu, mafua, kifua, kufunga choo, huimarisha misuli hasa ya wazee, husaidia shinikizo la juu na chini la damu na kusaidia afya ya mwili.

Pia kwa maradhi ya miguu na kifua tafuna mbegu zake, kwa maradhi ya malaria, chuma kilo moja, maji lita mbili na nusu chemsha kwa muda wa dakika 15, tumia nusu kikombe cha chai kutwa mara tatu kwa siku tano.

Pia hukinga maradhi ya saratani. Mchanganua huu umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu, www.dkmandai.com ili kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu afya zetu.

No comments:

Post a Comment