Monday, 21 May 2018

Baini maajabu ya kishona nguo katika tiba


Kishona nguo

KISHONA nguo ni mmea ambao unapatikana katika maeneo mengi nchini, licha ya kuwa kila sehemu au mkoa wenyeji wanauita kwa jina lao.

Mmea huu unapatikana mashambani lakini pia kwenye makazi ya watu mijini na vijijini.

Kwenye baadhi ya makabila majani ya kishona nguo ni mboga inayopendwa kutokana na utamu wake licha ya kuwa ina asili ya ladha ya uchungu.
Hata hivyo, mmea wa kishona nguo ni tiba nzuri kwa maradhi mengi ambayo jamii imekuwa ikihangaika kuyatafutia tiba.

Majani yake hutumika kutibu maradhi ya kisukari, tengeneza juisi yake kisha mpe mgonjwa glasi moja asubuhi na jioni kwa muda wa wiki mbili na zaidi, sukari yake itabaki katika hali ya kawaida.

Pia majani hayo yanatibu malaria, macho yenye ukungu, tatizo la kukojo kitandani, homa za vipindi kwa watoto, maradhi ya tumbo, minyoo, maambukizi ya njia ya mkojo (U.T.I), huondoa gesi tumboni na maradhi ya upungufu wa damu.

Kishona nguo pia ni mlinzi wa afya zetu kwa kuwa mmea huu una uwezo mkubwa wa kusafisha damu pengine kuliko mchicha.

Mwenye tatizo la shinikizo la chini la damu majani makavu yaliyokaushwa kivulini yanafaa sana kwa chai ambapo yatamsaidia kuondokana na tatizo hilo.

Matumizi ya majani ya kishona nguo pia yanasaidia kuepuka saratani ya utumbo mpana, bawasili na kuondoa sumu mwilini hasa zile zinazoambatana na chakula kwa kulisaidia ini na figo.

Maua yake yakikaushwa na kusagwa kuwa unga, yanafaa sana kwa kipodozi cha asili kwani huondoa chunusi na kulainisha ngozi.

Mmea huu wa ajabu babu zetu waliutumia pia kulinda ndoa zao ambazo nyingi zilidumu katika uhai wao wote.

Mchanganua huu umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana name kwa simu namba 0745900600 au tembelea website yetu kwa anwani www.dkmandai.com 

No comments:

Post a Comment