Wednesday, 16 May 2018

Baini namna chai ya mchaichai inavyosaidia matatizo mengi ya kiafyaMAJANI ya mchaichai ni maalufu katika maeneo mengi kwa kuwa yanatumika kutengenezea chai yenye harufu na radha nzuri inayopendwa na wengi.
Wengi wanatumia mchaichai kwa kuwa tu una radha nzuri bila kujua umuhimu mkubwa ulio ndani ya kinywaji hicho adhimu.
Mchaichai unasaidia mambo mengi sana katika miili yetu ambayo ni pamoja na kupunguza maumivu ya tumbo kwa kinamama wakati wa hedhi,  husaidia kusafisha figo, huzuia tumbo kunguruma, husaidia uyeyushaji chakula, hutuliza maumivu ya tumbo, hupunguza makali ya homa na ni msaada kwa wenye tatizo la baridi yabisi.
Pia hupunguza uwezekano wa kupatwa na maumivu mbalimbali ya mwilini. Tafiti kadhaa zinaonesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupambana na athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwa wenye vidonda.
 Wengine huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli.
Aidha, mmea huu ukipandwa katika nyumba huleta neema na baraka. Mchanganua huu umeletwa kwako na mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.
Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana na mtaalam Mandai kwa simu namba 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment