Saturday, 19 May 2018

Benki ya Azania kuwasaidia wanawake kuelekea mapinduzi ya uchumi wa viwanda

Meza kuu wakiimba wimbo wa taifa.


Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka 'Princess of Africa' akimtambulisha mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe. Benki hiyo ndiyo mdhamini mkuu wa Kongamano la Kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' lililofanyika Dar es Salaam.


Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe, akiwasalimia washiriki wa Kongamano la Kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' lililofanyika jijini Dar es Salaam. 


Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka 'Princess of Africa' akitoa mada wakati wa Kongamano la Kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika (African Women in The 4 Industrial Revolution in Tanzania) lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka 'Princess of Africa' akitoa mada katika kongamano hilo.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo. 

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo. 


Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' akitoa mada katika Kongamano hilo.


Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa kongamano hilo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, akimpongeza mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' baada ya kutoa mada katika kongamano hilo.


Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' akiimba pamoja na Ally Kiba. 


Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' akiimba pamoja na msanii wa Bongo Fleva Ally Kiba 'King Kiba'. Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, akitoa mada katika kongamano hilo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, akitoa mada wakati wa kongamano hilo.

Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Azania, Jackson Lohay (katikati), akifuatilia kongamano hilo pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo.


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Gaudensia Kabaka (katikati), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe. 


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ambaye alikuwa mgeni rasmi akisoma hotuba yake wakati wa kongamano hilo.


Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Amina Salum Ali, akisoma hotuba yake wakati wa kongamano hilo.Mmoja wa washiriki wa Kongamano la Kuwainua Wanawake Kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Benki ya Azania, Diana Balyati (katikati), alipotembelea banda la benki hiyo. 


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe, akizungumza na waandishi wa habari katika Kongamano la Kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika, lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na benki hiyo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa benki hiyo, Diana Balyati (kulia) alipotembelea banda la benki hiyo katika kongamano la 'Africa Reconnected Forum'.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Modester Maziba (kushoto), na kulia ni Meneja Masoko, Diana Balyati, kabla ya kuanza Kongamano la Kuwainua Wanawake Kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na benki hiyo. BENKI ya Azania imedhamiria kuwasaidia wanawake katika kipindi hiki cha mapinduzi ya uchumi wa viwanda kwa kuwapatia mikopo mikubwa, ya kati na midogo kwa riba naafuu.

Akizungumza Dar es salaam katika kongamano la kuwainua wanawake kuelekea katika Mapinduzi ya Nne ya Viwanda barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' Mkurugenzi Mtendaji wa Azania ambao ndio wadhamini wakuu wa kongamano hilo, Charles Itembe amesema wanawake ni kundi muhimu katika kufikia uchumi wa viwanda.

Amesema katika kuhakikisha hilo linafanikiwa pamoja na kukabiliana na hali ya soko ilivyo wameshusha riba za mikopo kwa wafanyabiashara hao.

"Benki nyingi sio sisi tu zimeshusha riba za mikopo hii ni kutokana na hali ya soko, na huenda zikaendelea kushuka hadi pale itakapoonekana imekuwa sawa kulingana na Benki yenyewe" amesema Itembe.

Aidha, amesema benki hiyo itaendelea kuwasaidia wanawake wanaojihusiha na kilimo kwani ndio kinategemewa katika kuzalisha malighafi za viwandani na kuongeza kuwa kikitumiwa vizuri uchumi wa kati utafikiwa kwa wakati.

No comments:

Post a Comment