Saturday, 5 May 2018

Binti mfalme Mohamed bin Rashed al- Maktoum hajulikani alipoKIKUNDI cha kutetea haki za binadamu chenye kuongoza harakati za wapi alipo binti mfalme, kimehimiza mamlaka za Dubai kufumbua fumbo la wapi alipo binti wa mtawala wa Emirate,Mohammed bin Rashed al-Maktoum.
Inaarifiwa kuwa binti mfalme Latifa alikuwa katika jaribio la kutoroka kasri na nchi yake ili kwenda kuishi maisha huria nje ya mipaka ya ufalme.
Ingawa mashuhuda wanadai kuwa boti ya kifahari aliyokuwa anasafiria ilivamiwa na maofisa wa kulinda usalama wa Pwani katika bahari ya Hindi, na baada ya hapo walimkamata binti huyo na kumrejesha Dubai, tangu wakati huo hajulikani aliko.
Mohamed bin Rashed al Maktoum
Maofisa wa ufalme waliiambia BBC kuwa hawawezi kuzungumzia chochote kuhusu sakata la binti mfalme kutokana na sababu za kisheria na kuongeza kuwa wanaowashikilia walikuwa na historia ya shughuli za jinai.

No comments:

Post a Comment