Friday, 18 May 2018

Bungeni jijini Dodoma jana Mei 17, 2018

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kigwangala (kushoto) na mbunge wa Karagwe,  Innocent Bashungwa wakiwa pamoja na Mwanamitindo wa Kimataifa, Flaviana Matata (katikati) kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata  wakati  alipomtembelea jana bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akimskiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati wa  kikao cha 31 cha mkutano wa kumi na moja cha Bunge hilo jana jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa  kikao cha 31 cha mkutano wa 11 wa Bunge jijini Dodoma. (PICHA ZOTE JUU NA DAUDI MANONGI-MAELEZO)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Madini, Angela Kairuki, Bungeni jijini Dodoma jana.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo, Bungeni jijini Dodoma jana.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jaffo akizungumza na mbunge wa Mikumi, Joseph Haule, Bungeni jijini Dodoma jana.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile,  akijibu swali, Bungeni mjini Dodoma jana.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,  akijibu swali, Bungeni jijini Dodoma, jana Mei 17, 2018.
  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akifurahi jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jaffo, Bungeni jijini Dodoma, jana Mei 17, 2018.

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, akizungumza Bungeni mjini Dodoma jana Mei 17, 2018. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akisalimiana na mbunge wa Hanang, Mary Nagu, Bungeni jijini Dodoma jana Mei 17, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia, Bungeni jijini Dodoma, Mei 17, 2018. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment