Saturday, 5 May 2018

Daraja la Magufuli lazinduliwa Kilombero


Daraja la Magufuli

Claudia Kayombo

RAIS Dk. John Magufuli leo amezindua daraja jipya la Kilombero ambalo kuanzia sasa litaitwa daraja la Magufuli.

Daraja hilo lililozinduliwa mchana huu lina urefu wa zaidi ya mita 300, ni miongoni mwa madaraja matano makubwa nchini, mengine ni pamoja na lile la Mkapa na la Nyerere lililopo Dar es Salaam.

Kabla ya uzinduzi huo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbalawa amesema kwa mamlaka aliyokuwa nayo ameona ni vema daraja hilo liitwe la Magufuli.

Amefafanua kuwa hilo limekuja baada ya Rais Magufuli kuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha ujenzi huo tangu alipokuwa waziri wa ujenzi kabla ya kuchaguliwa kuwa rais.

Kabla ya kuzinduliwa Rais Magufulia alisema kuzinduliwa daraja hilo linalounganisha wilaya ya Ifakara na Malinyi kutarahisisha usafiri baini ya mkoa huo na mingine ukiwemo Ruvuma.

Amesisitiza watanzania kushikamana kwa kuwa maendelea hayana chama na kwamba yeye ni rais wa watanzania wote bila kujali itikadi za vyama, rangi wala dini.

No comments:

Post a Comment