Saturday, 26 May 2018

Dawa zenye asili ya Asia zinasaidia kukabiliana na magonjwa mengi


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai

KUMEKUWA na ongezeko la watu wanaosumbuliwa na maradhi ya maumivu ya kifua, mawe katika figo, matatizo ya uzazi kwa kinababa na kinamama na maumivu ya viungo.

Kuishi mazingira yenye baridi kali na kutokupenda kunywa maji ya kutosha ni miongoni mwa sababu zinazochangia maumivu ya kifua na mawe katika figo.
Ili kukabiliana na magonjwa hayo tumia shimal, kamuni abiambwi, zamda na alihinji.

Bidhaa hizi zenye asili ya Asia, changanya kisha twanga au saga, unga wake utumie katika maji moto, changanya na asali vijiko vikubwa viwili nakijiko cha chai cha unga huo au tumia katika uji mwepesi.

Kinamama wanaosumbuliwa na maradhi ya tumbo yanayosababishwa na hedhi au wenye tatizo la kibofu cha mkojo dawa hii pia husaidia sana.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment