Sunday, 20 May 2018

DC Lushoto awataka madiwani kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo yao

 Mkuu wa wilaya ya Lushoto, January Lugangika akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Bumbuli ambacho kwa mara ya kwanza kilifanyika eneo la makao makuu Kwehangara.


Mkurugenzi wa halmashauri ya Bumbuli, Peter Nyalali akizungumza katika kikao cha robo ya mwaka cha Baraza la Madiwani kilichofanyika eneo jipya ambalo ni makao makuu ya halamshauri hiyo, Kwehangala. Wa pili kulia ni mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Amiri Sheiza.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Bumbuli, Amiri Sheiza akizungumza katika kikao hicho kwa kuwataka wananchi kuwa wamoja kuhakikisha halmashauri hiyo inapata mafanikio. Kushoto kwake ni mkurugenzi wa halmashauti ya Bumbuli, Peter Nyalali.

Mkurugenzi wa halmashauti ya Bumbuli, Peter Nyalali kushoto akiwa na mwenyekiti wa halmashauri ya Bumbuli ,Amiri Sheiza wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye kikao hicho.

Mkuu wa wilaya ya Lushoto, January Lugangika kulia akipitia makabrasha wakati wa kikao hicho.

 Sehemu ya madiwani wakifuatilia kikao hicho.

Sehemu ya wananchi waliopata fursa ya kuhudhuria baraza hilo.
 


MKUU wa wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga January Lugangika amewataka madiwani wa halmshauri ya Bumbuli kuhakikisha wanashiriki kukagua miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali ili kuepusha kujengwa chini ya kiwango na hivyo kukosa tija kwa wananchi.

Agizo hilo amelitoa juzi wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kawaida cha robo tatu kilichofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu mapya ya halmashauri hiyo eneo la Kwehangara.

Amesema iwapo madiwani hao watashindwa kukagua miradi hiyo inatoa mwanya kwa wakandarasi kushindwa kuitekeleza kwa viwango vinavyotakiwa hali inayopelekea kukosa tija na thamani halisi ya fedha zinazotumika. 

“Ndugu zangu madiwani hakikisheni mnakagua miradi ya maendeleo hili ndilo jukumu lenu la msingi kwani msipofanya hivyo ndipo wakandarasi wanafanya miradi hiyo isiwe na tija na hivyo matokeo yake gharama inayotumika inakosa thamani yake,” amesema DC Lugangika.

Aidha pia amemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo ,Peter Nyalali kuweka utaratibu mzuri kwa madiwani ili waende kukagua miradi inayotekelezwa hususan miradi ya maji ambayo imekuwa ikihujumiwa kutokana na wakandarasi," amesema. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Bumbuli, Amiri Sheiza aesema wanamshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kuwatatulia mambo mawili makubwa.

Ametaja mambo hayo kuwa ni ujenzi wa jengo la halmashauri eneo la Kwehangara na pili ni ufunguzi wa kiwanda cha Mponde.

Katika mambo hayo ameonesha namna ambavyo anatujali, hivyo tunamuomba Mungu amwongezee hekima na busara katika kuiendesha nchi na pia napenda kumthibitishia Rais kwamba wananchi, Baraza la Madiwani pamoja na kupishana kifikra bado tupo pamoja kufanya kazi bila kubaguana,” amesema.

Hata hivyo, ameonya kuwa mtu ambaye ataanzisha maneno kuhusu suala hilo watamchukulia hatua kali kwa sababu atakuwa hana nia njema na wananchi wa halmashauri hiyo katika kuwaletea maendeleo.

“Nionesha mtu yoyote atakayeleta vimaneno kuhusu suala hili sisi hatutamvumilia tutamchukulia hatua kali kwani wana Bumbuli na mbunge wetu sote pamoja," amesema.

No comments:

Post a Comment