Wednesday, 2 May 2018

Hafla ya ACT Wazalendo kupokea wanachama wapya Dar es Salaam

Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, mkoa wa Dar es Salaam, Salim Sudi akizungumza wakati wa hafla ya kuwapokea wanachama wapya 118 waliojiunga na chama hicho kati ya Januari na Aprili mwaka huu mkoani Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika juzi Temeke ambapo Katibu mkuu wa chama hicho Taifa, Doroth Semu alikuwa mgeni rasmi


Baadhi ya wanachama wa ACT Wazalendo wakionesha kadi zao mara baada ya kukabidhiwa na Katibu mkuu wa chama hicho, Doroth Semu.


Wanachama wa ACT Wazalendo wakiwapungia mikono wenzao wa chama hicho (hawapo pichani), baada ya kukabidhiwa kadi zao juzi Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho, Doroth Semu.


Katibu mkuu wa ACT Wazalendo, Doroth Semu akimkabidhi mmoja wa wanachama wapya kadi ya chama hicho, katika hafla iliyofanyika juzi Temeke Dar es Salaam ambapo chama hicho mkoa wa dar es Salaam kimepata wanachama wapya 118 katika kipindi cha Januari na Aprili mwaka huu 2018.

No comments:

Post a Comment