Wednesday, 2 May 2018

Hata kama baridi ni chanzo cha maambukizi ya Ukimwi chukueni tahadhali – Magufuli


Rais Dk. John Magufuli

Claudia Kayombo

RAIS Dk. John Magufuli amesema hata kama baridi ndiyo inachangia kupaa kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi mikoa ya Njombe na Iringa wakazi wake wanatakiwa kuchukua tahadhali kwa kuwa Virusi vya Ukimwi ni janga.

Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Mei 2, 2018, mkoani Iringa baada ya kuzindua hospitali ya wilaya ya Kilolo.

“Ukimwi ni janga naomba tuchukue tahadhali, huenda baridi inachangia maambukizi haya makubwa, lakini tuchukue tahadhali.

“Kwa nchi nzima maambukizi ya Ukimwi yameshuka lakini mikoa ya Iringa na Njombe yamepanda, naomba tuchukue tahadhali ya kujikinga,” amesisitiza Dk. Magufuli.

Wakati huo huo, ametoa mwito kwa watanzania kujiunga na mifuko ya afya kwa ajili matibabu kwa kuwa ugonjwa huo haupigi hodi.

Amesema mtu akijiunga na bima ya afya atakuwa na uhakika wa matibabu bora wakati wowote atakapokumbwa na maradhi.

No comments:

Post a Comment