Tuesday, 29 May 2018

Haya ndiyo mavi ya tembo kiboko kwa watoto waliozaliwa na hitilafu


Mavi ya tembo

MAPOKEZI ya mtoto anapozaliwa yakikosa umakini kidogo tu yanasababisha apate hitilafu katika ubongo wake anapofikisha umri wa kuanzia miezi sita.

Mara nyingi umri huo hadi miaka miwili anaweza kuanza kuanguka licha ya hakupata homa kali iliyochangia tatizo hilo. Tatizo hilo linapojitokeza familia nyingi zimekuwa zikimbilia kumpa mafusho ambayo si mazuri kupewa mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 10.

Ni vema wanafamilia wanapobaini tatizo hilo kwa mtoto wao waende kwa madaktari bingwa wa magonjwa ya watoto ambao wanaweza kuwasaidia au baadhi ya wataalam wa tiba asili.

Tangu enzi za mababu zetu walitumia kinyesi cha tembo tena kile cha moto kukabiliana na tatizo hilo. Kinyesi cha mnyama huyo wa porini kichanganywe na mafuta ya mbono, nazi au nafaka nyingine kisha kumchua mwili mtoto mwenye tatizo hilo.

Pia apewe chakula chenye virutubisho kilichosheheni oksijeni na glucose ambacho kitakwenda katika ubongo wake kusaidia kuirudisha mishipa katika hali nzuri.

Chakula hicho ni muhogo, ulezi na mbegu za maboga ambapo kwa pamoja vichanganywe na kusagwa, mtoto atengenezewe uji mwepesi au hata mzito utamsaidia sana kuondokana na tatizo hilo.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment