Wednesday, 30 May 2018

Hii ndiyo lufwambo kiboko ya pumu


Mmea wa mlazalaza au lufwambo

PUMU (Athma), ni ugonjwa unaosababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa upumuaji.  Ugonjwa huu umekuwa ukiwapata watu wa rika na jinsia zote kwenye maeneo mbalimbali nchini na hata nje ya nchi.

Mtu anaweza kupata pumu iwapo atakuwa anakaa karibu na moshi au wakati mwingine anaweza kurithi kutoka kwa mmoja wa ndugu wa damu aliyewahi kukumbwa na maradhi hayo.

Wapo matabibu wa tiba za jadi ambao wamebobea katika kuwasaidia watu wanaohangaika kutafuta tiba ya maradhi mbalimbali yakiwemo yale yaliyoshindikana katika tiba za kisasa.

Mmea unaojulikana kama mlazalaza au lufwambo unaopatikana maeneo mengi hususan vijijini, ni msaada mkubwa wa maradhi hayo. 

Majani ya mlazalaza yenye ladha ya sukari, ndiyo hasa ni tiba ya pumu. Mmea huu hutoa mbegu zenye rangi nyekundu ambapo watoto wa vijijini huzitumia kwa kuchezea michezo yao kwenye mchanga.

Chukua majani mabichi ya mmea huu yenye uzito wa nusu kilo, yatwange kisha tengeneza juisi, changanya na mayai matatu ya kuku wa asili, vijiko vikubwa vitano vya asali na ndimu au limau mbili au tatu inategemeana na ukubwa changanya vizuri mchanganyiko huo.

Kunywa nusu glasi ya mchanyiko huo mara mbili asubuhi na jioni muda wa siku saba. Tiba hii pia inaweza kuondoa sumu mwilini na makohozi.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 pia tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment