Saturday, 19 May 2018

Hizi ndizo tende zinazoongeza nguvu za kiume na kupevusha mayai kwa kinamama


Tende
TENDE ni tunda maarufu zaidi nchini na maeneo mengine duniani hasa wakati huu wa Ramadhani kwa kuwa wengi wanatumia kufuturu.

Tunda hili utamu, lina faida nyingi katika mwili wa mlaji kwa kuwa lina kiwango kikubwa cha sukari na nyuzinyuzi (fibre), inayohitajika kumpa nguvu mfungaji.

Tende pia inasaidia uyeyushaji haraka wa chakula tumboni, huondoa maradhi ya tumbo na matatizo ya kutopata choo pamoja na kunguruma.

Kinababa wenye tatizo la nguvu za kiume tende zinasaidia kuwaongezea nguvu na hivyo kuwafanya wadumu katika tendo hilo kwa muda mrefu zaidi.

Hiyo inatokana na ukweli kwamba tende zina uwezo mkubwa wa kusukuma damu hadi kwenye uume na kutoa mbegu nyingi.

Si wanaume peke yao, hata wanawake kwanza kwa wanaonyonyesha zinawasaidia kuwa na maziwa ya kutosha kwa watoto wao lakini pia husaidia kupevusha mayai.

Unaweza kutumia mbegu tatu za tende pamoja na glasi moja ya maziwa freshi ukafanya hivyo asubuhi na jioni au ukatengeneza juisi ya tende na kunywa ni nzuri kwa kuwa ina faida nyingi kwa mwili wa binadamu.

Mchanganua huu umeletwa kwako na mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana na mtaalam Mandai kwa simu namba 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment