Wednesday, 30 May 2018

Ijue nguvu ya mimea tiba kwa machango ya kinamama


Mwanamke anayekabiliwa na maumivu makali ya tumbo yanayosababishwa na chango.


KUNA aina nyingi za machango ya uzazi yanayowasumbua kinamama hata wale ambao wamekoma muda wao wa kuzaa. Lipo chango la kumwaga, la kukata na la kutapika.

Msoloka pia ni tatizo jingine kama hilo ambalo kinamama hutokewa na kitu kama puto au yai na kuziba njia ya uzazi, mara nyingi linawatia fadhaha kubwa wanawake ambao linawatokea. 

Mara nyingi machango hayo yanaambatana na maumivu makali ya tumbo, humfanya mwanamke kukosa raha asipopata tiba ya kueleweka.

Mababu zetu walijua changamoto hizo kubwa wanazokumbana nazo wanawake, hivyo, walitumia tiba asili za mimea kusaidia matibabu ya maradhi hayo.

Chukua vipingili vya mti wa muomboa ambao mara nyingi huota maeneo ya milimani vichemshe pamoja na vile vya mti wa myege kunywa maji yake kikombe kimoja cha chai asubuhi na kingine jioni, maji ya dawa yanayobaki safishia sehemu za siri.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 pia tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment