Friday, 11 May 2018

Jani la katikati la mgomba linavyosaidia tatizo la kwikwiTATIZO la kwikwi kama yalivyo maradhi mengine limekuwa likiwakumba baadhi ya watu katika jamii zetu kila siku. Wataalam wanasema tatizo hilo linatokana na ukosefu wa maji mwilini.  Linawakabili watu wa rika zote. Mara nyingi wengi wanalihusisha na nguvu za giza kwa maana ya kuwa wamelogwa.

Kabla ya kuingia tiba za kisasa, zamani babu zetu walitumia tiba za mimea kuwasaidia watu wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya. Mimea hiyo tunayo hadi sasa ambayo inaweza kutatua tatizo la kwikwi.

Tatizo hili linaweza kuondoka kwa kutumia mimea iliyojifunga, kama jani la katikati la mgomba wa ndizi ambalo ni miongoni mwa dawa hizo.

Namna ya kutumia

Twanga jani la katikati la mgomba ambalo limejifunga changanya na maji kidogo, juisi yake weka makaa matatu ya moto kisha mnyweshe mgonjwa kwa kutumia bunda la mpapai (kipande chenye tundu kati ya shina la mpapai na jani)

Wakati wa kumywesha mgonjwa anatakiwa awe ndani mnyweshaji nje ambapo dawa itoke nje kupitia bomba imfikie mgonjwa aliye ndani. Wakati anakunywa mtu mwingine amwite mgonjwa naye aitike kisha ameza funda la dawa hadi inapokwisha.

Kwa mwenye tatizo asisite kuja makao yetu makuu ambapo atapata maelezo ya kina ya namna sahihi ya kutumia mmea huu ili kuondokana na tatizo lako la kwikwi na mengine.

Mchanganuo huu umeletwa kwako nami Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment