Sunday, 20 May 2018

Jifunze haya kuepuka kifo cha mapema


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akionesha moja ya mimea tiba katika kitabu.

SIKU zote tunapopambana na magonjwa lengo ni kutaka tubaki salama licha ya kuwa tunajua kuwa kila mtu lazima afe, hilo lipo hata katika vitabu vitakatifu kwa maana ya Koran na Biblia.

Tunataka mtu afe si kwa sababu ya uzembe fulani bali ni baada ya yeye mwenyewe kuishia maisha ya kuepuka visababishi vya vifo visivyo vya lazima.

Hata hivyo, kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuchangia mtu kufa haraka moja likiwa ni kutofanya ibada. Kufanya ibada daima kuna mweka mtu karibu na Mungu wake na hivyo kuwa amani rohoni na hivyo kufanikiwa kutekeleza malengo yake ya msingi.

Kuwa mbali na Mungu kunazua hofu na hivyo kuwa ni moja ya sababu ya msingi inayoweza kupelekea kifo ca mapema cha mtu husika.

Sababu ya pili ni kukaa sehemu moja kwa muda mrefu iwe ni ofisini au eneo jingine lolote la kazi, hali hiyo inaweza kusababisha maradhi yasiyo ambukiza kama moyo, kisukari na figo.

Inashauriwa mtu kuepuka kukaa eneo moja kwa zaidi ya saa tatu vinginevyo pata muda wa kutembea kidogo kisha rudi kuendelea na kazi yako.

Sababu ya tatu na nne kuishi bila furaha au kuwa mpweke. Mtu hukosa furaha baada ya kujikataa kwa kujihisi kuwa ni mbaya wa sura, maskini wa hali au hakubaliki na jamii inayomzunguka.

Hilo ni baada  ya mtu huyo anapokuwa mbele ya jamii na kutoa mawazo yake humbezwa, hali hiyo huzua humkosesha furaha na amani na hivyo kumweka katika hatari ya kufa mapema.

Sababu ya tano ni kula vyakula visivyo na lishe inayohitajika katika mwili wa binadamu kama visivyo na makundi ya vyakula kama protini, wanga, vitamini na mafuta.

Ni vema jamii izingatie kula mlo wenye makundi mchanganyiko ya vyakula ili kuupa mwili mahitaji muhimu kuuepusha na magonjwa yasiyo ya lazima.

Sababu ya sita kuangalia kitu kimoja kama televisheni kwa muda mrefu wa kuanzia saa nne na zaidi. Mtu huyo anaweza kufa haraka kwa sababu mwili wake utatengeneza kiwango kikubwa cha sumu na hivyo kuwa katika hatari ya kupata maradhi ya shinikizo la damu, figo na hata kisukari.

Sumu hiyo inatokana na mafuta na sukari iliyoko mwilini kutounguzwa baada ya mwili kutulia bila kujihusisha na chochote.

Sababu ya saba kulala au kutolala kwa muda mrefu. Kwa kawaida mtu mzima anapaswa kulala kwa muda wa saa 8 hadi 9, ukilala saa tatu unakuwa ni sawa na mtu aliyekunywa kreti moja la bia.

Hali hiyo ikiendelea kwa muda mrefu unakuwa katika hatari ya kufa mapema. Kulala usingizi kwa muda unaotakiwa ni jambo muhimu la kuongeza uhai wa binadamu.

Kulala sana nako ni hatari mwili unajikusanyia kiwango kikubwa na mafuta na hivyo kunakuweka katika hatari ya kupata maradhi mengi ambayo yanaweza kukuondoa mapema.

Sababu ya nane ni kuishi kwa hofu. Hofu kwa binadamu inatokana na sababu nyingi, lakini huwa inamwondolea amani na furaha hali ile inatoka fursa kwa nyongo kutema sumu nyingi ambayo itamsababishia magonjwa ya kumwondoa mapema.

Sababu ya tisa ni kuishi bila mpenzi. Kwa kawaida mwanadamu yeyote kuanzia miaka 20 awe mwanamke au mwanaume anatakiwa kuwa na mwezi wa jinsia tofauti.

Mwezi huyo atamsaidia kuondoa sumu katika moyo kwa kuwa atakuwa ni sehemu ya faraja kwake. Mfano ni pale mke au mume anapokuwa dukuduku na hivyo kumweleza mwenza wake na hivyo kuondokana na sumu ya moyo,lakini pia kuondokana na uzito wa jambo linalombua.

Mtu ambaye mtu una uwezo wa kumweleza jambo lako hata liwe la siri inasaidia kukuepusha na kifo cha mapema.

Mchanganua huu umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea website yetu upate mambo mengi zaidi kwa anwani ya www.dk mandai.com.

No comments:

Post a Comment