Friday, 25 May 2018

Jiji la Dodoma lapewa mwezi kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya Hombolo


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo akikagua moja ya jengo lilijengwa katika kituo cha afya cha Hombolo kilichopo katika jiji la Dodoma leo kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa kituo hicho.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo akikagua jengo la maabara wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya cha Hombolo kilichopo katika jiji la Dodoma leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo akitoa maagizo kwa uongozi wa jiji la Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Hombolo leo, 2018.


Baadhi ya wananchi wa Kata ya Hombolo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo (hayupo pichani) akiongea katika ziara ya kukagua ujenzi wa Kituo cha afya cha Hombolo kilichopo katika Jiji la Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na wananchi wa Hombolo( hawapo pichani)  wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya Hombolo kilichopo katika jiji la Dodoma leo.

Angela Msimbira

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(Tamisemi), Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa jiji la Dodoma kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha Hombolo ifikapo mwishoni mwa Juni.
Jafo ametoa agizo hilo leo wakati alipotembelea kituo hicho kinachojengwa kwa gharama ya milioni 500 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na mtoto, chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kuhifadhia maiti na  nyumba ya mtumishi .
Jafo amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho kwa kuwa ni wiki 16 sasa zimepita na bado kituo hakijakamilika.
“Naelekeza kuwa ifikapo mwishoni mwa Juni, 2018 kazi iwe imekamilika na wananchi wa Hombolo waweze kupata kituo kizuri cha afya cha kuhudumiwa,” amesema Jafo.
Amewataka wataalamu wa jiji la Dodoma kuhakikisha wanasimamia kwa weledi ujenzi wa kituo hicho ili kiendane na thamani ya fedha inayotolewa na Serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Ni jukumu la wataalam kusimamia kwa uadilifu miradi ya maendeleo kwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya nchini,  ni vyema kazi itakayofanyika iendane na thamani ya fedha zinazotolewa,” amesema.
Amewataka wananchi kulinda na kusimamia miundombinu ya vituo vya afya nchini badala ya kuiachia Serikali kwa kuamini kuwa ndiyo yenye jukumu ya kuilinda.
Aidha, ameagiza  jiji la Dodoma kuhakikisha  hadi kufikia  Desemba, 2018 taasisi zote za Serikali zinapatiwa hati miliki kwa kuwa  ndio wenye dhamana ya kuzitoa.

No comments:

Post a Comment