Sunday, 6 May 2018

Juisi ya kitungu maji inasaidia kuondoa mba mwiliniJuisi ya kitunguu maji

MBA wa mwili mara nyingi hushamiri hasa sehemu za shingoni na usoni. Mba huu kitaalam unajulikana kama ‘tinea versicolor’.

Tiba

Tumia glasi moja ya juisi ya kitunguu maji kutwa mara tatu kwa muda wa siku 10 hadi 14.

Mwarobaini na ndizi mbivu

Chemsha mwarobaini, kisha changanya maji yake na ndizi mbivu iliyopondwa pondwa vizuri.

Paka mwili mzima nusu saa kabla ya kuoga asubuhi na jioni kwa muda wa wiki mbili.

Mdalasini na asali

Vijiko viwili vya unga wa mdalasini changanya na vingine viwili vya asali, koroga vizuri, paka mchanganyiko huo sehemu zote zenye mba. Endelea kila siku jioni kwa muda wa wiki moja.

Limau

Paka maji ya limau moja ukiwashwa sehemu za siri, ni fangasi, tumia kujisafisha na maji ya limao ukichanganya na maji safi na miguuni pia paka vidoleni.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment