Tuesday, 22 May 2018

Kamati ya kuratibu mchakato wa serikali kuhamia Dodoma yakagua jengo jipya la Takwimu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, ambaye ndiye anayesimamia Kamati inayoratibu mchakato wa serikali kuhamia Dodoma akifafanua jambo wakati walipokagua jengo jipya la Takwimu. Kulia kwake ni  Katibu Mkuu wa ofisi yake, Maimuna Tarishi na kushoto kwake ni  katibu wa kamati hiyo, Meshach Bandawe, jana Mei 21, 2018, jijini Dododma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akipata maelezo ya ukumbi wa mkutano katika  jengo jipya la Takwimu kutoka kwa Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo, Mhandisi, Abdulkarim Msuya, jana Mei 21, 2018, jijini Dododma.

Muonekano wa jengo jipya la Takwimu, ambalo linamilikiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na limejengwa na Kampuni ya Ujenzi  ya Hainan International, jana Mei 21, 2018 jijini Dodoma. Katika kufanikisha azma  ya serikali kuhamia Dodoma, Serikali inaboresha miundombinu ya barabara, reli, uwanja wa ndege, umeme, mifumo ya maji safi na maji taka, ofisi, makazi na kuimarisha huduma za elimu, afya, mawasiliano na michezo.

Mwandishi wetu
 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Walemavu), Jenista Mhagama ambaye ni  msimamizi wa Kamati inayoratibu mchakato wa serikali kuhamia Dodoma na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi pamoja na katibu wa kamati hiyo, Meshach Bandawe wamekagua jengo jipya la Takwimu, linalo milikiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu lililojengwa  na Kampuni ya Ujenzi  ya Hainan International.
 
Katika kufanikisha azma  ya serikali kuhamia Dodoma, Serikali inaboresha miundombinu ya barabara, reli, uwanja wa ndege, umeme, mifumo ya maji safi na taka, ofisi, makazi na kuimarisha huduma za elimu, afya, mawasiliano na michezo.
 
Serikali imejipanga kuijenga Dodoma kuwa jiji bora na la kisasa linaloendana na mahitaji na mifumo ya majiji bora duniani. Ili kufikia azma hiyo, Serikali inashirikiana na wadau ikiwemo sekta binafsi na mashirika ya kimataifa kulijenga jiji la Dodoma.
 
Aidha, katika hatua nyingine, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye mara tu baada ya kuhamia Dodoma amezindua “Kampeni ya Kijanisha Dodoma” inayolenga kuifanya Dodoma kuwa ya kijani. 
 
Serikali inaendelea kutekeleza mchakato wa kuhamishia shughuli za Serikali Kuu Dodoma. Tangu utekelezaji wa mchakato huo uanze Septemba 2016, watumishi wa umma 3,829 kutoka Wizara na taasisi mbalimbali wamehamia Dodoma katika awamu ya kwanza na ya pili, na awamu ya tatu inaendelea.

No comments:

Post a Comment