Wednesday, 9 May 2018

Kampuni ya Ulinzi ya SGA yafurahia ushindi

 Meneja wa kampuni ya ulinzi ya SGA, Daudi Mungi aliyeshika kikombe
akifurahi na wafanyakazi wenzake katika hafla ya kuwapongeza wafanyazi
bora iliyofanyika ofisini kwao Esso jijini Arusha, walitangazwa washindi
wa kwanza katika kundi la watoa huduma wakati wa maadhimisho ya Mei
Mosi, mkoa wa Arusha.

Wafanyakazi wa kampuni binafsi ya ulinzi ya SGA wakifurahia kikombe cha
mshindi wa kwanza kwa taasisi zinazotoa huduma ofisini kwao eneo la Esso
jijini Arusha.
 
 

  Mwandishi Wetu, Arusha


KAMPUNI binafsi ya ulinzi ya SGA imewapongeza kwa kuwapa vyeti wafanyakazi wake 20 walioshiriki matembezi ya Siku ya Wafanyakazi duniani yaliyofanyika kimkoa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Katika hafla ya kuwapongeza iliyofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo eneo  Esso jijini hapa, meneja wa kampuni hiyo, Daudi Mungi amesema ni tukio la aina yake kwa kampuni hiyo tangu ianze kazi zake hapa nchini kupata kombe.

“Tumekua wenye furaha sana kuzawadiwa kombe la mshindi wa kwanza katika kundi letu, hili tukio linalotupa chachu ya kuongeza bidii kwenye utendaji wa kazi zetu na kuhakikisha wateja wetu wanakuwa salama,”amesema Mongi.

Katibu wa chama cha wafanyakazi wa Chodawu mkoa wa Arusha,Jeremia Meliari amesema ushindani katika kundi hilo ulikua mkali na kuwapongeza kwa ushindi walioupata.

Amewataka waongeze tija kwa kutoa huduma bora kwa wateja wao na kuifanya kampuni hiyo kukua zaidi na kutoa fursa za ajira kwa vijana wengi ili wasijiingize kwenye vitendo vya uhalifu.

No comments:

Post a Comment