Tuesday, 8 May 2018

Kavumbasi ina nguvu ya kufukuza mapepo, majini

Mvumbasi

MATABIBU wanatumia mimea tiba ya aina mbalimbali kutibu watu wanaokabiliwa na matatizo ya kiafya.

Moja ya mimea wanayotumia ni pamoja na kavumbasi wengine wanaita mwinula huku watani zangu wangoni wakiita manunganunga. Mmea huu unasaidia matatizo mengi ya kiafya ambayo yameshindikana hospitali.

Ukifanikiwa kumwona mtaalamu wa tiba ya mimea akakupa maelekezo mazuri ya namna sahihi ya kutumia unasaidia sana. Kuna aina mbili za mmea huu ambao harufu yake hufukuza mbu pia na wenye kimo cha futi mbili hadi tatu.

Kuna kavumbasi jike na dume. Kavumbasi dume hukua zaidi ya jike, una majani mapana wakati jike haukui sana na majani si mapana kulinganisha na ya dume.

Unaweza kukausha mbegu na maua yake kisha kujifusha pepo au jini iwapo alikuandama atatoweka, na kwa wale wanaojisikia homa majira ya saa za jioni kata majani yake pika kisha jifukize mapepo, majini na nguvu za giza iwapo kama ilikuwa ni sababu kuumwa vinatoweka.

Ukitwanga (kusaga) majani ya kavumbasi yaliyokauka na ukaweka katika uji mwepesi au maji moto inamsaidia siku za hedhi kuwa na mpangilio maalum kwa yule aliyekuwa na tatizo hilo.

Pia mjamzito anaweza kujifungua bila kufanyiwa upasuaji iwapo majani yake akayachanganya katika mboga akala au unga wa majani yake akautumia katika uji mwepesi au majimoto.

Kwa mwenye tatizo asisite kuja makao yetu makuu ambapo atapata maelezo ya kina ya namna sahihi ya kutumia mmea huu kuondokana na matatizo yanayokusumbua.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata maelezo ya kina.

No comments:

Post a Comment