Friday, 25 May 2018

Kiharusi si maradhi ya kulogwa- Mandai


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia maradhi ya kiharusi.


UGONJWA wa kiharusi unatokea baada ya damu kwenda isivyo kawaida katika ubongo. Athari za ugonjwa huo ni pamoja na mgonjwa kupooza upande mmoja, viungo kama mdogo au mkono kwenda pembeni au hata kupoteza maisha.

Hata hivyo, mara nyingi maradhi haya yanapomtokea mwanajamii wengi wanaamini kuwa amepigwa na jini au pepo hivyo kuchelewa kumkimbiza hospitali kupatiwa matibabu.

Ni vema mtu anapopatwa na kiharusi asitingishwe, akandwe taratibu viungo vyake kwa mafuta ya mbono, ya kitunguu swaumu au ya nazi kuruhusu damu kupita katika sehemu zote za mwili kisha akimbizwe hospitali.

Baada ya hapo atumie mchanganyiko wa alikisusi, karafuu, kamuni aswedi, dalfilfil, kazubalaa, maua maulidi na kachili ni mujarabu sana kwa ugonjwa huu.

Kiharusi kingine mtu huanguka chooni ambapo anaweza kupoteza maisha au fahamu. Kama nilivyosema hapo awali maradhi haya mara yanapotokea imani za kishirikina hutawala.

Mtu anayeanguka chooni hali hiyo inatokana na tatizo la mzunguko wa damu kupata hitilafu kwa kuwa tukio la kujisaidia alichutama na kutumia nguvu nyingi hivyo anapoinuka damu nayo huenda kwa kasi sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo katika ubongo na hivyo kusababisha tatizo hilo.

Jambo la msingi jamii izingatie maelekezo ya wataalam kuhusu magonjwa mbalimbali ili kuiokoa jamii na madhara yanayoweza kujitokeza kwa mgonjwa kuchelewa kupatiwa tiba.

Mchanganua huu umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu, www.dkmandai.com ili kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu afya zetu.

No comments:

Post a Comment