Friday, 18 May 2018

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani awatahadharisha watawa kuhusu matumizi ya mitandao

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ametoa waraka wa kuwataka watawa kutumia mitandao ya kijamii kwa tahadhari.
Waraka huo umetaja mawasiliano ya mitandao ya kijamii, badala ya kusema application husika, lakini Gazeti la kikatoliki limesema application hizo zimemaanisha Facebook na twitter.
Amri ya watawa Kaskazini mwa Hispain ilisambaa na kuwa kwenye vichwa vya habari kwenye mitandao ya kijamii mwezi uliopita kuzungumzia kesi iliyokuwa na mkanganyiko mjini Pamplona iliyoeleza kundi la wanaume waliokuwa wakishutumiwa kubaka ambapo watu walidai kuwa hukumu haikuwa kali dhidi ya wanaume hao.
Katika ukurasa wao wa Facebook, watawa wa Hondarribia walimtetea mwathirika wa ubakaji kwa kuelezea uamuzi huru wa kuishi maisha ya utawa wa kutokunywa pombe au kutembea nyakati za usiku.
“Kwa kuwa ni uamuzi huru, tutatetea kwa namna yoyote tutakayoweza. Haki ya wanawake kuwa huru kutenda kinyume bila kuhukumiwa, kubakwa, kutishiwa au kudhalilishwa kutokana na makosa yake.
Muongozo huu mpya haujatolewa kutokana na kesi hiyo, na hii si mara ya kwanza Kanisa Katoliki kutoa miongozo kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watawa.
Katiba ya asili kuhusu maisha ya wanawake watawa, ilichapishwa mwaka 1950 na Papa Pius wa 12, lakini Papa Francis katika toleo la mwaka 2016 ametahadharisha utamaduni wa digitali na namna unavyoathiri jamii.
Amewataka watawa wasifanye mitandao ya kijamii kuwa vitu vya kupotezea muda akisema Vatican yenyewe huandika sana kwa kutumia mtandao wa Twitter.
Imeweka karibu jumbe 15,000 kwenye anuani yake mpya ya habari na kuweka zaidi ya mara 1,500 kupitia ukurasa maalumu wa Baba Mtakatifu.
Pia Vatican ina anuani za mtandao wa Facebook,Instagram,You Tube na Google+.

No comments:

Post a Comment