Friday, 4 May 2018

Kiongozi wa upinzani Msumbiji afariki


KIONGOZI wa muda mrefu wa Chama cha upinzani Renamo cha nchini Msumbiji, Afonso Dhlama amefariki dunia baada ya kushambuliwa na maradhi ya moyo.
Dhlakama ameongoza Renamo katika kipindi cha miaka 15 ya uasi dhidi ya serikali ya Msumbiji, kilichomalizika mwaka mwaka 1992.
Amefariki dunia akiwa na miaka 65. Alikuwa akiungwa mkono na serikali iliyokuwa ikiongozwa na Wazungu nchini Afrika Kusini na baadaye kuja kuwa Rhodesia.
Chama cha Renamo kilikuwa kikilaumiwa kwa mauaji ya watu wengi na kuwatumia watoto vitani.
Baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, Renamo kikawa chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji, wafuasi wake wameendelea kupambana na majeshi ya serikali.

No comments:

Post a Comment