Friday, 11 May 2018

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe akana madai ya udhalilishaji
Nelson Chamisa kushoto na Rais EmmeKIONGOZI wa upinzani nchini Zimbabwe ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa anapata tabu kuona amekosea wapi baada ya kusema kuwa atamtoa dada yake mwenye umri wa miaka 18 kama zawadi kwa Rais Emmerson Mnangagwa ikiwa atashinda asilimia tano ya kura.
Nelson Chamisa, aliyechukua uongozi wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) mwanzoni mwa mwaka huu, amejikuta matatani baada ya kauli hiyo kunaswa kwenye kamera.
Akizungumza kwa lugha ya Shonna, amesema alikuwa na furaha kuweka dau ''kwa sababu nilijua haitatokea''.
Lakini akizungumza na BBC, alikana shutuma za kuwa amefanya kitendo cha udhalilishaji wa kijinsia, shutuma zilizosambaa kwenye vyombo vya habari.
Utovu wa nidhamu kivipi? yeye ndiye anayetafuta mume. Ni dada yangu, hakuna udhalilishaji hapo, kwa ninavyofahamu hii ni sehemu ya utamaduni wetu. Dada yako anapokaribia kuolewa, kama kaka ni sharti umsaidie.''

No comments:

Post a Comment