Saturday, 19 May 2018

Kisamvu ni mboga na ni tiba

KISAMVU ni moja ya mboga za majani ambayo haipendwi na kila mtu. Mboga hii inasaidia mambo mengi katika mwili wa binadamu, ikiwa ni pamoja na kuwa uwezo mkubwa wa kuongeza damu pengine kuliko aina nyingine yoyote ya mboga za majani.

Mboga hii ina protini nyingi na kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi  (fible), inasaidia wanawake wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo wakati wa hedhi (chango).

Hata hivyo, kwa mjamzito inashauriwa asitumie juisi ya mboga hii ila kwa maelekezo ya tabibu kwa kuwa ina kiwango kikubwa cha kemikali inayoweza kumsababishia mimba kutoka.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la maumivu ya tumbo wakati wa hedhi, aponde mboga hii kisha aianike, ikikauka asage unga na kuutumia katika uji mwepesi au maji moto.

Juisi ya kisamvu husaidia wale wenye makohozi yanayoonekana kuwa katika koo muda wote, chukua kisamvu kiponde kisha kamua maji yake changanya na asali kunywa inaondoa tatizo hilo.

Pia mbegu za muhogo ambao ndiyo chanzo cha kisamvu, zikisagwa unga wake utumiwe katika uji mwepesi au maji moto unasaidia kuzibua mirija ya uzazi na kupevusha mayai.

Kwa mwenye maradhi ya kisukari atumie pia katika uji itasaidia kukiweka katika hali ya kawaida.

Mchanganua huu umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au nipigie simu kwa namba 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.  

No comments:

Post a Comment