Sunday, 6 May 2018

Kiwanda cha dawa za binadamu M-Pharmaceuticals chawekewa jiwe la msingi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kulia), akishirikiana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa tatu kulia) Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wanne kulia) na Mkurugenzi wa kampuni za IPP Reginald Mengi (watano kulia) kuzindua uwekaji wa jiwe la msingi la kiwanda cha dawa za binadamu unaotarajiwa kuanza hivi karibuni, ikiwa ni katika juhudi za ukuzaji sekta ya viwanda nchini. Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (watatu kulia), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wapili kulia) ,Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo(wakwanza  kulia), Mkurugenzi wa kampuni za IPP, Reginald Mengi (wanne kulia) na viongozi wengine wakimsikiliza mtaalamu wa michoro, Ruchir Sharma akielezea na kuonesha ramani ya kiwanda cha dawa kinachotarajiwa kujengwa eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo baada ya Waziri Ummy kuweka jiwe la msingi wa ujenzi huo. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa sherehe ya uwekaji jiwe la msingi la kiwanda cha dawa za binadamu Kerege kinachomilikiwa na Reginald Mengi,ambapo aliwahakikishia wawekezaji wazawa katika sekta ya afya kupata ushirikiano kutoka serikalini. Hafla hiyo imefanyika  wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi la kiwanda cha dawa za binadamu  kinachomilikiwa na Reginald Mengi, kilichopo Kerege, wilayani Bagamoyo, ambapo aliwahakikishia wawekezaji wazawa katika sekta ya viwanda na uwekezaji  kupata ushirikiano kutoka serikalini. Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.

Mwenyekiti mtendaji wa kampuni za IPP, Reginald Mengi akizungumza wakati wa sherehe ya uwekaji jiwe la msingi kiwanda cha dawa za binadamu kilichopo Kerege wilayani Bagamoyo, Pwani ambapo alishukuru ushirikiano alioupata kutoka serikalini wakati wa mchakato wa uanzishwaji wake.

Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, kutoka kulia ni mkuu wa gereza la Bagamoyo, Muyengi Machumu, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Malisa Emmanuel na mkuu wa Polisi wilaya ya Bagamoyo, Adam Maro, wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(hayupo pichani) wakati wa kuweka jiwe la msingi kiwanda cha dawa za binadamu Kerege.


Wasanii kutoka Chuo cha Sanaa Bagamoyo wakitoa burudani wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda cha dawa za binadamu ambapo ujenzi wake unaoatarajiwa kuanza hivi karibuni katika eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. (PICHA NA ABUBAKARI AKIDA)

No comments:

Post a Comment