Friday, 25 May 2018

Kula karanga ni kinga dhidi ya saratani


Karanga

MBEGU za karanga huwa na kiasi kikubwa cha mafuta cha kati ya asilimia 38 hadi 50. Zimesheheni protini, kalisium, potashiamu, fosiforasi, magnesiamu na vitamini.
Karanga ni zao maarufu duniani, licha ya kuwa hapa nchini uzalishaji wake ni wa chini kutokana na kutokuwa na mvua za uhakika na kiwango kidogo cha teknolojia.
Miongoni mwa faida nyingi, inasaidikiwa kuwa karanga zina aina fulani ya viini vinavyotumika kama dawa. Zinaliwa zikiwa mbichi, zimechemshwa au kukaangwa.
Kitiba kama nilivyodokeza hapo juu, karanga ni dawa nzuri tena ni mlinzi wa moyo maana hazina lehemu (cholesterol). Ulaji wa karanga una kulinda na aina fulani ya saratani.
Ukila karanga pamoja na sukari gulu ya mgando inajenga kinga na ulinzi dhidi ya mashambulizi ya maradhi ya ini na kifua kikuu. Inakisiwa kuwa ratili moja ya karanga (nusu kilo) ina calories 3000, ndiyo maana inapendekezwa mafuta yake kuwa ni mazuri kwa kupikia.
Kula karanga wastani wa kiganja cha mkono wako kwa siku ni nzuri kwa maradhi ya kisukari.
Hata hivyo, licha ya kuwa karanga ni nzuri, kwa wanaougua maradhi ya jongo (gout) na matumbo dhaifu wanapaswa kuepuka kula kwani zinapokaangwa hutoa uric ambayo inaweza kuudhuru mwili.
Mchanganua huu umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu, www.dkmandai.com ili kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu afya zetu.

No comments:

Post a Comment