Monday, 7 May 2018

Magufuli awataka wanafunzi kuacha fujo vyuoni


Rais Dk. John Magufuli akiwa mkoani Morogoro

Claudia Kayombo

RAIS Dk. John Magufuli amewaonya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kutojiingiza katika mkumbo wa kuleta migomo kwani wakifanya hivyo hataogopa kuwafukuza shule.

Ametoa kauli hiyo leo Mei 7, 2018 wakati akihutubia wanafunzi, wahadhiri na wafanyakazi wa kada mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.

“Nikisikia mnaleta fujo sitaogopa kuwafukuza, na nikiwafukuza sijui nitawarudisha lini,” amesisitiza Dk. Magufuli.

Amesema anakipenda chuo hicho zaidi kwa kuwa pia kimepewa jina la Waziri mkuu wa zamani, Hayati Edward Sokoine ambaye alichukia rushwa, ufisadi na vitendo vyote vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Aidha, amesema anakusudia kutimiza dhamira njema aliyonayo baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere ya kuanzisha chuo hicho na kwamba katika awamu hii anataka itimie na hivyo kuwa cha mfano kitakachobadilisha maisha ya watanzania wengi.

No comments:

Post a Comment