Saturday, 12 May 2018

Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi wakiagwa rasmi kwa gwaride maalum

Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda wakiwaaga maofisa na askari Polisi huku wakisukumwa katika gari maalumu wakati wa gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi ndani ya jeshi hilo. Gwaride hilo lilifanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam.
 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akizungumza na IGP mstaafu Omar Mahita wakati hafla maalum ya kuwaaga  makamishna wastaafu wa jeshi hilo, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam. 

Kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake wakati wa hafla maalum ya kumuaga baada ya kustaafu utumishi ndani ya jeshi hilo. Hafla hiyo ilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam.

Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla maalum ya kuwaaga rasmi jeshini baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam.

Askari wa Kikosi cha Kutuliza ghasia (FFU) wakitoa heshima wakati  wa gwaride maalam la kuwaaga makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda baada ya kustaafu utumishi ndani ya jeshi hilo. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akifurahi jambo na makamishna wastaafu Clodwing Mtweve (katikati) na Elice Mapunda (kushoto) wakati wa hafla maalum ya kuwaaga baada ya kustaafu utumishi ndani ya jeshi hilo. Hafla hiyo imefanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (PICHA ZOTE NA JESHI LA POLISI).

No comments:

Post a Comment