Tuesday, 8 May 2018

Maofisa wanyamapori Uganda wamsaka chui aliyemla mtoto


Chui
MAOFISA wanyamapori nchini Uganda wanamsaka chui aliyemla mtoto wa kiume wa mwangalizi wa hifadhi ya taifa ya Queen Elizabeth.
Mtoto huyo, Elisha Nabugyere mwenye umri wa miaka mitatu, aliuawa na chui huyo, Ijumaa usiku, Shirika la habari la Ufaransa limeripoti. Alikutana na chui huyo wakati anamfuata mlezi wake nje ya nyumba za wafanyakazi ambazo hazina uzio.
“Msaidizi hakujua kama mtoto alikuwa akimfuata. Alimsikia akipiga kelele akiomba msaada. Alijitahidi kumuokoa lakini alikuwa amechelewa kwani chui alishatokomea naye, msako ulianza siku ya pili tulipata fuvu la motto,” msemaji wa mamlaja ya hifadhi nchini Uganda Bashir Hangi amesema na kuongeza.
“Msako unaendelea ili kumpata chui na kumuondoa kwenye hifadhi kwa sababu kwa kuwa amekula nyama ya binaadamu, shauku ya kuendelea kula wengine itaongezeka, hivyo amekuwa mnyama hatari.

No comments:

Post a Comment