Friday, 18 May 2018

Maua ya mwembe kiboko kwa wanawake wenye uchache wa maziwa


Maua ya mwembe

MAKABILA mengi yanapanda miembe kwa ajili ya matunda. Matunda ya miembe yanayojulikana kama embe, ni maarufu sana hapa nchini.

Ladha tamu ya embe bila shaka ndiyo inaongeza umaarufu wa tunda hilo na hivyo jamii kubwa zaidi kulistawisha kwa wingi zao hilo lenye majani yenye rangi ya kijani.

Zipo aina nyingi za embe ambazo hutofautiana kwa umbo na rangi ambapo zipo zile zenye rangi ya kijani haya zinapowiva, nyingine njano na hata nyekundu

Embe linaweza kuwiva likiwa juu mtini lakini kutokana na uharibifu unaotokana na ndege, wakulima wanayaangua baada ya kukomaa. 

Wanagundua embe limekomaa kutokana na rangi yake ya uchanga kubadilika.
Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai anasema mwembe una faida nyingi kuanzia matunda, majani, shina na maua.

Anasema majani ya mwembe yanatibu maradhi ya pumu na harufu mbaya ya mdomo pia yana uwezo wa kutibu malaria sugu.

“Chukua majani ya mwembe yakaushe katika kivuli ili kutoiondoa alkaloids iliyomo ndani ya majani hayo ambayo ni muhimu sana katika tiba.

“Unaweza kuwa mtanashati lakini kama una tatizo la kutoa harufu katika kinywa thamani yako inapungua,”anasema Mtaalam Mandai.

Kwa wanawake wanaonyonyesha lakini wanakabiliwa na tatizo lauhaba wa maziwa maua ya mwembe ni suluhisho.

Anasema chukua unga wa maua ya mwembe changanya na maji moto au asali au maziwa kunywa tatizo hilo linakwisha.

Pia embe lenyewe pamoja na faida nyingine linasaidia tendo la usanisi wa chakula tumboni.

Mchanganua huu umeletwa kwako na mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana na mtaalam Mandai kwa simu namba 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment