Friday, 11 May 2018

Maziwa ya nguruwe kiboko ya mleviULEVI umekuwa ni chanzo cha umaskini katika baadhi ya familia. Hii ni baada ya wakuu wa kaya hususan baba kutumia fedha nyingi katika kulewa badala ya kuhudumia familia.

Kimsingi pombe ikinywewa kwa kiasi ni lishe kwa mwili lakini pia ni tiba. Kutokana na ulevi watu wamejikuta katika changamoto mbalimbali za kimaisha.

Hata hivyo, ushirikina umekuwa sababu kwa baadhi ya watu kujikita ndani ya dimbwi la ulevi. Huenda baadhi ya watu wanaweza wasinielewe kwa kuwa tu nimezungumzia uchawi, lakini siwalazimishi wakubaliane nami ila wajue kwamba hata vitabu vitakatifu vimezungumzia jambo hilo, mashehe, wachungaji, mapadri na maaskofu wanafundisha waamini wao namna ya kuepukana na nguvu za giza.

Wakati baadhi ya walevi wakiwa kero katika familia, maziwa ya nguruwe na mnanaa ni tiba ya kudhibiti tatizo hilo.

Namna ya kutumia

Chukua maziwa ya nguruwe nusu glasi changanya na vijiko vitatu vya juisi ya mnanaa baada ya kuutwanga, kisha mpe mlevi anywe. Hii inasaidia sana kwa wenye tatizo hilo.

Kwa mwenye tatizo asisite kuja makao yetu makuu ambapo atapata maelezo ya kina ya namna sahihi ya kutumia mchanganyiko huu ili kuondokana na tatizo la ulevi.

Mchanganuo huu umeletwa kwako nami Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment