Saturday, 12 May 2018

Mbaazi mmea wa ajabu unaokinga na kutibu matatizo mengi katika jamii


Mbaazi zikiwa shambani

MBAAZI ni mmea asili ambao wazee wetu waliutumia kama kinga majumbani pia kutibu maradhi mbalimbali.

Kwa ujumla mmea huu ni msaada kwa mambo mengi, ukiuweka ndani ya nyumba ni kinga inayoweza kupambana na watu wabaya, majani yake yanaharibu na kukinga ubaya.

Wenye tatizo la hedhi isiyo ya kawaida, watumie jani la mbaazi lenye sehemu tatu baada ya kuponda na kupata juisi, itie katika kifuu cha nazi kisafi, tia kaa la moto kisha kunywa asubuhi kabla ya kula chochote.

Kimsingi kinamama wanatakiwa kwenda hedhi kati ya siku tatu hadi tano, inapozidi au kupungua linakuwa ni tatizo linalohitaji kupatiwa kufumbuzi.

Pia unaweza kuchukua robo kilo ya mbaazi changanya na kiasi kama hicho cha mtama, saga pamoja, tumia unga wake kila asubuhi kabla ya kula chochote katika maji moto au uji mwepesi unarekebisha hali hiyo.

Si hayo tu, mbaazi ukikauka watu huuweka ndani unasaidia kufukuza nguvu za giza. Pia unapokwenda sehemu unajua kuwa kuna nguvu za giza unaweza kuweka kipande cha mti huu mfukoni huwezi kudhurika.

Mizizi ya mbaazi inasaidia wenye maradhi ya kaswende, gonolea, wanaume wenye tatizo la kushindwa kutoka mkojo na hata wenye UTI.

Chukua mizizi ya mbaazi kiasi cha kujaa mkono mmoja, osha vizuri kisha chemsha kwa muda wa dakika 15, kunywa kikombe kimoja cha chai kutwa mara tatu.

Naweza kusema kuwa dawa hii ni tiba nzuri kwa magonjwa ambayo yameshindikana hospitalini. Kwa mwenye tatizo asisite kuja makao yetu makuu ambapo atapata maelezo ya kina ya namna sahihi ya kutumia mmea huu.

Mchanganuo huu umeletwa kwako nami Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment